- 317 viewsDuration: 1:14Timu ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, Junior Starlets, imerejea nchini kutoka Afrika Kusini baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mkondo wa kwanza wa mechi za kufuzu Kombe la Dunia. Kikosi kinachonolewa na Mildred Cheche sasa kinaelekeza nguvu zake kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa Jumapili katika Uwanja wa Nyayo, Nairobi. Junior Starlets wanahitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Morocco mwezi Oktoba mwaka huu.