- 10,050 viewsDuration: 14:29Kafara ya amani: Ni zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu kasisi wa Kanisa Katoliki Allois Cheruyiot Bett auwawe kwa kupigwa risasi na majangili alipokuwa akieneza amani katika Bonde la Kerio, kaunti ya Elgeyo Marakwet. Kufikia sasa, hakuna mtu yeyote aliyekamatwa wala kushtakiwa kwa mauaji yake. Hata hivyo, kama Seth Olale anavyotu arifu katika makala ifuatayo, mbali na safari ya familia ya kutafuta haki, watu 16 waliokuwa majangili wa mifugo wakati wa juhudi za amani zilizoendeshwa na marehemu Kasisi Allois, wamesalimisha bunduki na risasi. Hii ni katika makala ya Kafara ya Amani.