- 504 viewsDuration: 1:07Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka sasa anasema wito wa Rais Ruto wa kutaka mazungumzo ya kitaifa kuendeleza maono ya mwaka wa 2030 hauna maana yoyote. Kalonzo badala yake amesema kuwa serikali inapaswa kushughulikia masuala muhimu yanayowaathiri Wakenya, hasa kwa upande wa uchumi. Ameendelea kuishambulia serikali kwa kukosa uongozi wa kuridhisha. Kalonzo alizungumza katika kaunti ya Embu leo wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa la All Saints Peter's ACK Cathedral.