Kamati ya bunge la kitaifa kuhusu nyumba, ujenzi na mipangilio ya miji imesema nyumba za bei nafuu zinazojengwa kaunti ya Kwale pamoja na soko la Mvindeni, zinatekelezwa kulingana na matarajio ya bunge na kwa manufaa ya mwananchi.
Akizungumza baada ya kuongoza kamati hiyo kukagua baadhi ya miradi eno la Matuga na Diani, mwenyekiti wa kamati hiyo Mugambi Rindikiri amesema jumla ya shilingi bilioni 14 zilizowekezwa kenye miradi hiyo zimeinua uchumi wa kaunti hiyo kwa kubuni nafasi za ajira kwa vijana na akina mama.