Skip to main content
Skip to main content

Kamati ya usalama Kisumu yaonya wanasiasa kuhusu mipango binafsi ya usalama

  • | Citizen TV
    1,110 views
    Duration: 2:22
    Kamati ya usalama katika kaunti ya Kisumu imewaonya wanasiasa dhidi ya kupanga ulinzi wa kibinafsi wakati wa mikutano ya kisiasa ili kukabiliana na visa vya uhuni. Akizungumza leo, Kamishna wa Kaunti ya Kisumu Mohamed Mwabudzo amesema serikali ina maafisa wa kutosha kuhakikisha usalama katika mikutano hiyo. Agizo hilo linajiri kufuatia malalamishi kuhusu kudorora kwa usalama jijini Kisumu.