- 202 viewsDuration: 2:05Serikali imetakiwa kuangazia upya mgao wa bajeti katika sekta ya afya ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa kote nchini. Wakizungumza kule kimilili kwenye kambi ya matibabu kwa wagonjwa wasiojiweza, wadau wa afya wamesikitikia idadi kubwa ya wagonjwa wenye maradhi mbalimbali huku wengi wakishindwa kumudu gharama ya juu ya matibabu . Kwenye hafla hiyo zaidi ya wagonjwa 500 walipata matibabu bila malipo kutoka kwa wataalamu wa afya kutoka hospitali mbalimbali .