Skip to main content
Skip to main content

Kampeni dhidi ya mihadarati Kajiado

  • | Citizen TV
    182 views
    Duration: 2:08
    Maafisa wa Serikali ya Kaunti ya Kajiado wametamaushwa na ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa vijana, hali inayozidi kuathiri maisha yao. Kupitia kampeni ya “Kick Drugs Out of Kajiado” inayoendeshwa na shirika la ODARI kwa ushirikiano na Serikali ya Kaunti, vijana wanahamasishwa kuacha mihadarati kupitia michezo ya kandanda, pamoja na kupokea ushauri nasaha wa afya ya akili. Akizungumza wakati wa michuano iliyofanyika Isinya, Mratibu wa NACADA kaunti ya Kajiado Nyambura Kigera alisema pombe haramu na bangi bado ndizo zinatumiwa kwa wingi, akionya kuwa uraibu wake unachangia pakubwa matatizo ya afya ya akili miongoni mwa vijana.