- 12,541 viewsDuration: 2:41Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa maafisa watakaokuwa kazini wakati endapo mfungwa atapatikana amefariki kwenye seli. Akikashifu kuongezeka kwa visa vya mauaji vituoni na utovu wa nidhamu miongoni mwa baadhi ya maafisa wake, Kanja amesema makamanda wa polisi pia wataadhibiwa kwa kukosa kuwadhibiti maafisa wanaohusika na visa hivi vya uhalifu.