- 177,277 viewsDuration: 3:21Waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Lodwar, Kaunti ya Turkana, wameshangazwa na kisa ambapo jamaa aliyedai kuwa kasisi alitambuliwa kuwa bandia. Inadaiwa kuwa jamaa huyo aliyejiwasilisha katika jimbo hilo wiki tatu zilizopita alidai kuwa kasisi kutoka Tanzania akisema alikuwa likizoni. Alipewa majukumu ya kuendesha misa mara kadhaa kabla ya askofu wa jimbo hilo kugundua kuwa hakuwa kasisi. Na kama anavyoarifu Cheboit Emmanuel, inadaiwa kuwa jamaa huyo alitumia stakabadhi ghushi na kwamba ana mke na watoto Kisii.