- 654 viewsDuration: 2:00Kasisi Mkuu katika Kanisa la All Saints, Provost Evans Omollo, ameitaka serikali kuchukua hatua ya kukomesha wanaodaiwa kuwafadhili wahuni. Akizungumza katika mahojiano ya Daybreak asubuhi ya leo, Omollo amefichua kuwa kuna njama ya kuzima kesi dhidi ya wahuni waliovuruga mkutano katika All Saints Cathedral wiki iliyopita. Aidha, amesema wale walioandikisha taarifa polisi wameshinikizwa kubadili nia yao.