- 7,117 viewsDuration: 1:04Maafisa wa polisi Katika kaunti ya Nakuru,wameanzisha uchunguzi kufuatia mauaji ya kasisi wa kanisa la PCEA Tabuga, Lanet, eneo Bunge la Bahati. Kasisi huyo aliuawa usiku wa kuamkia leo na genge la majambazi alipokuwa Katika ua la kanisa hilo. Marehemu amekuwa akiishi katika boma hilo kwa miaka minne ambayo amehudumu Katika Parokia ya Tabuga. Polisi wakisema mauaji hayo yalifanyika mwendo wa Saa nane usiku wa kuamkia leo, huku bawabu akinusurika na majereha. Bawabu huyo anapokea matibabu Katika hospitali ya Rufaa ya Nakuru.