- 8,521 viewsDuration: 4:02Katibu wa Wizara ya Vijana na Michezo, Fikirini Jacobs, ameandikisha taarifa kuhusiana na kifo cha kijana Cecil Ouma, aliyepigwa risasi kwa njia tata ndani ya gari linalohusishwa naye katika Barabara ya Park Road, Nairobi. Fikirini, aliyefika katika makao makuu ya polisi kutoa taarifa yake, amesema anashirikiana na maafisa wa upelelezi kufuatia tukio hilo. Haya yanajiri huku ripoti ya upasuaji wa maiti ikionyesha kuwa Ouma alipigwa risasi moja iliyoingia kwenye pafu na kukwama kwenye uti wa mgongo.