- 15,999 viewsDuration: 9:03Katibu wa idara ya petroli Mohamed Liban, Mkurugenzi mkuu wa Kenya Pipeline Joe Sang na Mkurugenzi Mkuu wa EPRA Daniel Kiptoo wamejiuzulu kutoka kwenye nyadhifa zao siku moja baada ya kukamatwa kuhusiana na sakata ya uagizaji wa mafuta. Hatua za kinidhamu pia zimeanzishwa dhidi ya naibu mkurugenzi wa idara ya petroli Joseph Wafula, na meneja wa usambazaji wa KPC Joel Mburu. Taarifa kutoka kwa afisi ya Rais William Ruto zimesema watano hao wanadaiwa kubadilisha ripoti ya kuwepo kwa mafuta nchini kwa nia ya kuongeza bei ya mafuta.