- 621 viewsDuration: 2:09Katibu katika idara ya uwekezaji na viwanda nchini Abubakar Hassan Abubakar anasema kuwa jumla ya shilingi bilioni 9 zimewekezwa kaunti ya kilifi na wawekezaji katika sekta ya viwanda katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Akizungumza katika eneo la Sabaki gatuzi ndogo ya Magarini kaunti ya Kilifi wakati wa ufunguzi rasmi wa kiwanda cha kutengeneza sharubati, Abubakar anasema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa kaunti ya Kilifi ilikuwa na viwanda 10 pekee lakini katika kipindi cha miaka mitatu viwanda 14 zaidi vimezinduliwa na kubuni nafasi elfu 14 mpya ikilinganishwa na elfu kumi zilizokua hapo awali.