Serikali za kaunti za Kisumu, Siaya na Vihiga vimeanza mchakato wa kudhibiti uharibifu wa chakula, haswa maboga yanayochukua muda mrefu sokoni. Chini ya mradi unaofadhiliwa na shirika la UNEP, wachuuzi na wakulima watahusishwa katika ukusanyaji wa vyakula hivyo, ili kugawanyia shule za chekechea. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, uzinduzi huo unajari wakati ambapo takwmu zinaonyesha kuwa asilimia arobaini ya vyakula vinavyozalishwa humu nchini huharibika kutokana na ukosefu wa miundombinu ya uhifadhi.