- 132 viewsDuration: 2:24Serikali za kaunti zimehimizwa kuimarisha ushirikiano na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ili kuboresha utoaji wa huduma, hususan katika sekta ya afya. Wito huo umetolewa Kaunti ya Kilifi wakati wa hafla ya kupokea vipakatalishi 19 pamoja na pikipiki kutoka LVCT Health. Vifaa hivyo vinatarajiwa kuimarisha matumizi ya teknolojia, ukusanyaji na usafirishaji wa data kutoka vituo vya afya mashinani, pamoja na kurahisisha usafiri wa wahudumu wa afya.