- 11,019 viewsDuration: 3:18Viongozi wa Kenya kwanza kwa mara nyingine wamemfokea aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua dhidi ya majigambo ya matokeo ya uchaguzi mdogo wa Ol kalou wakisema, uchaguzi huo ulikuwa baina ya DCP na Jubilee na wala sio Kenya Kwanza. Wakizungumza eneo bunge la Lafey kaunti ya Mandera, viongozi hao akiwemo Waziri wa afya Aden Duale na Spika Moses Wetangula waliohudhuria hafla ya kupiga jeki makundi kujiwezesha wamesema mambo bado na Gachagua na wenzake wasubiri kivumbi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.