Kenya na Urusi zimeweka mkataba wa ushirikiano ili kuwawezesha raia wa Kenya wanaohusika katika operesheni za kijeshi nchini humo kujiondoa kwa hiari. Akiwasilisha ripoti bungeni kuhusu hali ya wakenya waliojiunga na jeshi la Urusi, Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi amefichua kuwa zaidi ya Wakenya 250 wanaaminika kujiunga na vikosi maalum vya Urusi katika vita vinavyoendelea vya Russia-Ukraine. Kulingana na ripoti hiyo, wakenya kumi wameuwawa, wengine 47 wakiokolea, huku wawili wakizuiliwa kama wafungwa wa kivita nchini Ukraine