Skip to main content
Skip to main content

Kenya U23 yailenga Tanzania baada ya ushindi wa 4-1

  • | Citizen TV
    2,434 views
    Duration: 45s
    Timu ya Kenya ya soka ya chini ya miaka 23, Emerging Stars, itamenyana na Tanzania kesho alasiri katika mechi ya marudiano ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika U23 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Kenya inaingia katika mchezo huo ikiwa na faida ya mabao 4-1 kutoka kwa mkondo wa kwanza uliochezwa katika Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi wiki iliyopita. RUN VCR Timu zote mbili zitakosa baadhi ya wachezaji kutokana na majeraha. Kenya itamkosa Jack Ong’aya, ambaye alipata jeraha la goti katika mkondo wa kwanza na baadaye kuondoka kambini kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kimatibabu. Tanzania pia inaingia katika mchezo huo ikihitaji ushindi wa angalau mabao matatu ili kugeuza matokeo ya mkondo wa kwanza na kusonga mbele. Kocha mkuu wa Tanzania, Ahmad Ally, amesema timu yake imechukua matokeo ya mchezo wa kwanza kama changamoto na inalenga kupigania nafasi ya kufuzu katika mchezo wa marudiano. Mshindi wa jumla kati ya Kenya na Tanzania atasonga hadi raundi ya pili, ambako atakutana na Ivory Coast.