- 1,362 viewsDuration: 3:23Kenya imezindua rasmi azma ya jaji wa Mahakama ya Upeo, Njoki Ndung’u, kuwania nafasi ya jaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ICC. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa azma hiyo katika Ikulu ya Nairobi, Rais William Ruto amesema uteuzi wa Jaji Njoki unaonyesha imani ya Kenya na mahakama hiyo ya kimataifa. Na kama anavyoarifu Emily Chebet, iwapo Jaji Njoki Ndung’u atachaguliwa, atajiunga na jopo la majaji 18 wa mahakama hiyo yenye makao yake The Hague nchini Uholanzi.