- 746 viewsDuration: 1:18Mwenyekiti wa Baraza la Waluo, Ker, Odungi Randa amewaonya watu wa jamii hiyo kujitenga na kile anachosema ni mwelekeo tofauti wa kisiasa wa jamii hiyo. Randa amesema kuwa wale wanaochukua mwelekeo huo watalaaniwa na wazee wa jamii hiyo. Akizungumza kwa lugha ya Kijaluo, Randa ameitaka jamii hiyo kusalia nyuma ya serikali na kuunga mkono kuchaguliwa tena kwa Rais Ruto.