- 1,683 viewsDuration: 51sVikao vya kusikiliza kesi ya uchunguzi kuhusu mauaji ya Rex Masai, aliyepigwa risasi wakati wa maandamano ya Gen Z mwaka 2024, vimekamilika baada ya miaka miwili. Mtaalamu wa uchunguzi wa kidijitali kutoka IPOA, Joshua Mutua, amethibitisha kuwa video za kamera za CCTV zilizowasilishwa kama ushahidi hazikufanyiwa mabadiliko yoyote. Mutua alimweleza Hakimu Geoffrey Onsarigo kuwa video hizo zilikabidhiwa IPOA kabla ya kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu. Jumla ya mashahidi 30 wa upande wa mashtaka walitoa ushahidi katika kesi hiyo. Pande husika sasa zitawasilisha hoja zao kwa maandishi, kabla ya hakimu kutoa uamuzi wake.