Skip to main content
Skip to main content

Kesi ya uuzaji wa hisa za Safaricom yaanza kusikilizwa

  • | Citizen TV
    347 views
    Duration: 1:15
    Kesi kuhusu uuzaji wa hisa za kampuni ya Safaricom imeanza kusikilizwa katika Mahakama Kuu huku upande wa serikali na washtakiwa ukitoa ushahidi wake mbele ya majaji Francis Gikonyo, Roselyne Aburili na Tabitha Ouya. Upande wa serikali ulisema kuwa uuzaji wa hisa hizo kwa kampuni ya Vodacom ulifanyika kwa kuzingatia matakwa yote ya kisheria. Hata hivyo, wapinzani wa mpango huo wakiongozwa na kinara wa Wiper na wakili Kalonzo Musyoka wamedai kuwa hatua hiyo itaipa Vodacom asilimia 55 ya hisa katika kampuni hiyo ya mawasiliano. Kalonzo amesema hatua hiyo inaweza kuhujumu usimamizi wa rasilimali za umma ikiwemo data za Wakenya.