- 2,271 viewsDuration: 2:02Kesi mbili tofauti zimewasilishwa mahakamani kupinga agizo jipya la Halmashauri ya Uchukuzi wa Barabarani (NTSA) kuhusu ukaguzi wa lazima wa magari. Kesi hizo zilizowasilishwa na kundi la kutetea haki za kibinadamu la Sheria Mtaani na kampuni ya sheria ya Mugane zimepinga kanuni mpya za ukaguzi wa magari wakisema maoni ya Wakenya hayakukusanywa kabla ya kutungwa kwa sheria hizo. Wamedai pia kuwa utekelezaji wa agizo hilo utawalazimu Wakenya kubeba gharama zaidi.