Skip to main content
Skip to main content

Kiambu yakusanya mapato ya rekodi ya Sh6.5 bilioni

  • | Citizen TV
    420 views
    Duration: 1:26
    Kaunti ya Kiambu imekusanya mapato ya shilingi bilioni 6.5 katika mwaka wa kifedha wa 2025/2026. RUN NATS Akizungumza wakati wa uzinduzi wa taarifa kuhusu hali ya mapato ya kaunti hiyo, Gavana Kimani Wamatangi amesema kuwa mapato ya kaunti hiyo yameongezeka kutoka shilingi bilioni 2.8 katika mwaka wake wa kwanza mamlakani hadi shilingi bilioni 6.5 mwaka huu. Gavana Wamatangi ameeleza kuwa ongezeko hilo limetokana na mageuzi katika mifumo ya ukusanyaji wa mapato, akibainisha kuwa fedha hizo zimewezesha maendeleo makubwa bila kutegemea fedha zinazotengwa na serikali kuu. Serikali ya kaunti hiyo imasema kuwa mafanikio hayo yametokana na kuboreshwa kwa mifumo ya ukusanyaji wa mapato na usimamizi bora wa fedha za kaunti.