Skip to main content
Skip to main content

Kikosi cha Linda Mwananchi kipinga ujenzi wa kituo cha Ebola, kitishia maandamano

  • | Citizen TV
    3,439 views
    Duration: 1:17
    Kikosi cha Linda Mwananchi kimepinga ujenzi wa kituo cha karantini ya Ebola cha raia wa Marekani nchini, kikisema mpango huo haupaswi kuendelea bila ridhaa ya wananchi. Viongozi wa kikundi hicho, waliotembelea kaunti ya Machakos, wamesema watawaongoza Wakenya katika maandamano ya kupinga ujenzi huo wakisisitiza kuwa usalama na maslahi ya wananchi lazima yapewe kipaumbele. Aidha, viongozi hao wameahidi kushirikiana na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka katika uchaguzi mkuu ujao, wakisema ushirikiano huo unalenga kuimarisha sauti ya upinzani nchini.