- 200 viewsDuration: 1:41Wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Nzoia wanaendelea kuibua maswali mazito kufuatia sintofahamu kuhusu fedha zilizotolewa na serikali kulipia madeni ya mishahara katika sekta ya sukari. Hivi karibuni, serikali ilitangaza kutoa shilingi bilioni mbili ili kusaidia kulipa mishahara ya wafanyakazi wa viwanda vya sukari. Hata hivyo, wafanyakazi wanadai kuwa pesa hizo hazijawafikia.