- 8,037 viewsDuration: 3:32Naibu Rais Kithure Kindiki kupitia wakili wake Muthomi Thiankolu ameiomba mahakama kutupilia mbali ombi la aliyekuwa mtangulizi wake Rigathi Gachagua la kutaka kulipwa fidia, akisema hatua hiyo itahujumu uamuzi wa Bunge la Seneti wa kumuondoa mamlakani. Hata hivyo, Gachagua kupitia mawakili wake amesisitiza kwamba alitimuliwa mamlakani bila kufuata sheria, akitaka mahakama kukosoa mchakato huo na pia kumlipa fidia. Seth Olale anaripoti zaidi kuhusu sakata hilo.