- 6,661 viewsDuration: 3:10Naibu rais Prof.Kithure Kindiki hii leo ameongoza maafisa wa serikali kukashifu matamshi ya mtangulizi wake Rigathi Gachagua kwenye ibada ya wafu ya mbunge wa Ol Kalou siku chache zilizopita. Kindiki ametaja usemi wa Gachagua kuwa ulikosa heshima na kwa niaba ya wanasiasa wote akaomba msamaha. Kauli ya Kindiki inajiri wakati viongozi wengine serikalini wakizidi kumshtumu kinara huyo wa DCP na wandani wake kwa kile walichokitaja ni kumkosea rais heshima.