- 1,141 viewsDuration: 1:21Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki ametangaza kuwa watengenezaji wa pombe zinazouzwa nchini Kenya watafanyiwa upya ukaguzi na uhakiki. Akizungumza katika eneo bunge la Lari, Kaunti ya Kiambu, Kindiki amesema hatua hiyo imechochewa na kuongezeka kwa pombe hatari zinazodaiwa kuhatarisha afya ya wananchi. Naibu Rais pia amewataka Wakenya kuondoa siasa katika vita dhidi ya pombe haramu nchini, akisema jukumu la kukabiliana na suala hilo linapaswa kuachiwa vyombo vya usalama pamoja na mashirika mengine husika ya serikali.