- 164 viewsDuration: 1:12Kirinyaga kaunti iko mbioni kujiunga na kaunti zinazokusanya zaidi ya shilingi bilioni moja katika mapato ya kila mwaka baada ya kurekodi ongezeko la asilimia 44 ya ukusanyaji wa mapato. Serikali ya kaunti imesema ongezeko hilo linatokana na kuimarishwa kwa mifumo ya ukusanyaji wa mapato na hatua mbalimbali za kuboresha usimamizi wa rasilimali za kaunti.