- 24,590 viewsDuration: 3:58KizaaZaa kilishuhudiwa leo katika lango kuu la kuingia Bunge la Seneti, ambapo baadhi ya maseneta wa Kamati ya Uhasibu walimvamia na kumlazimisha Gavana wa Samburu, Lati Lelelit, kuingia kwenye kituo cha polisi cha Bunge. Hii ni baada ya gavana huyo kukosa kufika mbele ya kamati hiyo kujibu maswali ya matumizi ya fedha katika kaunti yake. Maseneta walisitisha mjadala kuhusu nyongeza ya fedha kwa kaunti, wakitishia kuzuia fedha zozote kwenda kaunti hadi watakapowajibika na kufika mbele yao kujibu maswali.