- 6,367 viewsDuration: 2:59Kizaazaa kilishuhudiwa katika mtaa wa Kileleshwa jijini Nairobi baada ya Mwakilishi Wadi wa eneo hilo, Robert Alai, kuvuruga mkutano ulioongozwa na machifu. Wapelelezi sasa wanachunguza kisa hicho huku wakazi wakidai kuwa mmiliki wa kipande hicho cha ardhi ananuia kujenga zaidi ya vyumba 400, hatua ambayo wakazi na majirani wameipinga. Runinga ya Citizen ilifika eneo hilo kupata taswira kamili ya mkasa huo na kuzungumza na Mwakilishi Wadi wa Kileleshwa kuhusu suala hilo.