Skip to main content
Skip to main content

Kizaazaa Nyabisase wanafunzi wakimkataa mwalimu mkuu mpya

  • | Citizen TV
    23,301 views
    Duration: 2:31
    Kizaazaa kimeshuhudiwa leo katika Shule ya Upili ya Nyabisase, eneo la Bobasi, Kaunti ya Kisii, baada ya wanafunzi na walimu kurushiana mawe kufuatia utata wa uongozi. Inaarifiwa kuwa mzozo ulianza baada ya wanafunzi kumkataa mwalimu mkuu mpya aliyetumwa kuiongoza shule hiyo. Baadaye, wanafunzi hao waliteketeza bweni kwa moto. Maafisa wa polisi kutoka Nyamache wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo na kuwabaini waliohusika.