Upatikanaji wa huduma za mifugo bado ni changamoto kubwa kwa wafugaji nchini, hali ambayo mara nyingi huweka mifugo katika hatari ya magonjwa na kusababisha hasara kubwa kwa wafugaji.
Hata hivyo, wataalamu wa kilimo sasa wanakabiliana na changamoto hiyo kupitia kliniki tamba za mifugo zinazolenga kufikisha huduma katika maeneo ambayo ni vigumu kwa wafugaji kufika kwenye vituo vya matibabu.
Kwenye Kilimo Biashara wiki hii, Denis Otieno anaangazia namna mpango wa kliniki tamba unavyobadilisha usimamizi wa mifugo na kusaidia kupunguza hasara kwa wafugaji.