- 1,997 viewsDuration: 3:02Jaji Mkuu Martha Koome ameitaka Tume ya Uchaguzi na Mipaka IEBC kuwafutilia mbali wanasiasa wanaodaiwa kufadhili wahuni wanaovuruga amani, hasa katika mikutano ya kisiasa. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango mkakati na kalenda ya uchaguzi ya IEBC, Koome amesema baadhi ya wanasiasa wamewateka nyara Wakenya kupitia siasa za migawanyiko na machafuko. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon amewataka wanasiasa kupunguza joto la kisiasa na kuhimiza mazingira ya utulivu kuelekea shughuli za uchaguzi.