Skip to main content
Skip to main content

Ligi Kuu ya kandanda yasubiri hadi Septemba huku kesi zikisimamisha kuanza

  • | Citizen TV
    303 views
    Duration: 4:09
    Ligi Kuu ya kandanda nchini haitaanza angalau hadi mwisho wa mwezi Septemba huku kesi zilizowasilishwa katika mahakama za Nairobi na Murang'a zikisimamisha kuanza rasmi kwa ligi hiyo. Ligi Kuu nchini ilipangiwa kuanza Ijumaa, lakini hilo halitafanyika kwa wiki zingine nne. Mahakama Kuu ya Murang'a itatoa uamuzi kuhusu kesi ya kupuuza mahakama iliyowasilishwa dhidi ya maafisa wa Shirikisho la FKF. Shirikisho hilo pia limewasilisha hoja ya awali kwa mahakamani dhidi ya uamuzi uliobatilisha uamuzi wa mahakama ya migogoro ya michezo. Mahakama hiyo iliamua kuwa FKF ilifuata taratibu sahihi katika kubadilisha sheria za mwaka wa 2025 za ligi hiyo. Lakini Mahakama Kuu ilitoa amri ya kusimamishwa kwa ligi, na FKF haiwezi kutekeleza maamuzi yaliyoafikiwa hadi kesi iliyowasilishwa na Kariobangi Sharks itakaposikilizwa na kuamuliwa. Mahakama itasikiliza kesi hiyo tarehe 24 Septemba na ligi imesimamishwa kuanza hadi wakati huo.