- 30,335 viewsDuration: 3:25Viongozi wa Linda Mwananchi wameendelea kusisitiza azma yao ya kuhakikisha upinzani unasimamisha mgombea mmoja wa urais atakayemenyana na Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu ujao. Wakizungumza katika kaunti ya Transnzoia katika siku ya kwanza ya ziara ya eneo la magharibi viongozi hao wanasema mazungumzo yatafanyika kati ya Linda Mwananchi na wenzao wengine wa upinzani ili kufanikisha uteuzi wa kiongozi mmoja atakayepeperusha bendera ya upinzani.