- 675 viewsDuration: 3:17Chama cha wanasheria nchini LSK kinasema kuwa mgomo wa mawakili kulalamikia idara ya mahakama utaendelea licha ya shughuli kuonekana kuendelea katika mahakama kadhaa nchini. Hata hivyo, baadhi ya kesi zililazimika kuahirishwa kutokana na mgomo huu wa mawakili. Mwenyekiti wa LSK Charles Kanjama ameilaumu idara ya mahakama kwa kuwatishia mawakili dhidi ya kuendeleza mgomo huo unaolaumu mahakama kwa ufisadi miongoni mwa wafanyikazi wake wakiwemo majaji.