- 184 viewsDuration: 4:03Mfumo wa elimu wa CBE unaozingatia mafunzo yasiyo ya nadharia umekumbwa na changamoto nyingi kufuatia ukosefu wa maabara na vifaa vya kutosha. Ripoti kadhaa kutoka kwa washikadau katika sekta ya elimu zinaonyesha kuwa wanafunzi wa kwanza wa mfumo huo waliathirika zaidi huku wengi wao wakimaliza Gredi ya Tisa bila hata kuingia katika maabara ya sayansi au ya kompyuta. Hata hivyo, suluhisho linaonekana kujitokeza hasa kwa wanafunzi wa shule za mashinani kufuatia kuanzishwa kwa maabara tembezi zinazolenga kuboresha upatikanaji wa mafunzo ya vitendo.