- 358 viewsDuration: 3:36Maafisa wa usalama kutoka kaunti za Isiolo, Samburu na Marsabit wawapa washukiwa wa wizi wa mifugo siku tano kurejesha mifugo walioibwa katika wiki za hivi karibuni. Makataa hayo yalitolewa wakati wa mkutano uliowahusisha wazee na viongozi wa eneo hilo katika Kaunti ya Samburu. Mkutano huo ulilenga kudhibiti visa vya wizi wa mifugo na kukomesha migogoro katika mipaka ya kaunti hizo tatu.