- 4,828 viewsDuration: 17sKwa siku ya pili mfululizo katika maeneo ya Kiamaiko, Huruma na barabara ya Outering, waandamanaji waliendelea na maandamano ya kushinikiza serikali kumwachilia kijana Abdiazziz Duba Molo, anayejulikana kwa jina la utani Zizo, au kumfikisha mahakamani. Waandamanaji hao wanataka mamlaka kutoa msimamo kuhusu aliko kijana huyo na hatua za kisheria zinazochukuliwa dhidi yake.