- 10,973 viewsDuration: 3:06Madaktari na wahudumu wa afya nchini sasa wanataka kituo cha karantini na matibabu ya ebola kwa raia wa marekani kuanzishwa nchini DRC badala ya katika kaunti ya Laikipia humu nchini. Muungano wa madaktari unasema kuwa matibabu na udhibiti zinafaa kufanyika kwenye kitovu cha ugonjwa huo badala ya kuuhamisha katika mataifa mengine. Aidha madaktari wanaitaka serikali kuimarisha utayari wa taifa kukabiliana na ugonjwa huo iwapo utaingia nchini kando na kuimarisha ufuatiliaji mipakani na katika viwanja vya ndege.