- 941 viewsDuration: 2:56Mahakama itatoa uamuzi Ijumaa ijayo kuhusu iwapo mpango wa fidia kwa waathiriwa wa maandamano utaendelea au kusitishwa. Hii ni baada ya baadhi ya waathiriwa kuwasilisha kesi wakipinga waathiriwa 35 wa utekaji nyara na kutoweshwa kwa lazima kuondolewa kwenye orodha ya wafidiwa. Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu (KNCHR) imeunga mkono malalamishi hayo ikisema kamati inayoongozwa na Profesa Makau Mutua haina mamlaka ya kuwaondoa waathiriwa kwenye orodha iliyowasilishwa. Willy Lusige na taarifa hiyo.