- 16,784 viewsDuration: 2:06Mahakama imeamuru Chama cha Orange Democratic Movement kuanzisha upya mchakato wa kumwondoa Katibu wa chama hicho Edwin Sifuna. Hii ni baada ya Sifuna kuishtaki chama hicho katika Mahakama ya Kutatua Mizozo ya Vyama vya Siasa, akilalamikia kung’atuliwa kwake bila kupewa fursa ya kujitetea. Aidha mahakama imesisitiza kuwa chama hicho kiko huru kumtimua tena Sifuna mradi kifuate utaratibu unaofaa.