Skip to main content
Skip to main content

Mahakama yaruhusu mashahidi zaidi katika uchunguzi wa kifo cha Rex Masai

  • | Citizen TV
    1,075 views
    Duration: 2:29
    Mahakama ya Milimani imeruhusu Idara ya Huduma za Polisi (NPS) kuwasilisha mashahidi wanane zaidi katika uchunguzi unaoendelea kuhusu kifo cha Rex Masai, aliyepigwa risasi wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa mwaka 2024. Hakimu Mkazi Mwandamizi Geoffrey Onsaringo amesema ushahidi wa mashahidi hao unaweza kuwa muhimu katika kubainisha mazingira ya kifo hicho. Mahakama pia imekataa ombi la kumrejesha shahidi mmoja kutoa ushahidi kwa mara ya tatu. Miongoni mwa mashahidi watakaotoa ushahidi ni wawakilishi wa Kituo cha Udhibiti na Mawasiliano cha Polisi, Benki ya Absa, Makau Casino, Hospitali ya Bliss na International Life House. Aidha, mahakama imeiruhusu IPOA kuwasilisha mashahidi wawili wa ziada. Willy Lusige ana taarifa zaidi.