- 1,183 viewsDuration: 2:14Mahakama Kuu imesitisha kwa muda ujenzi wa mradi wa Ikulu Ndogo ya Meru katika Msitu wa Imenti hadi kesi iliyowasilishwa dhidi ya mradi huo itakaposikilizwa na kuamuliwa. Katika kesi hiyo iliyowasilishwa na mwanaharakati Francis Awino pamoja na walalamishi wengine watatu, Jaji Joseph Mboya Oguttu wa Mahakama ya Mazingira na Ardhi amesema kuwa kuendelea kwa mradi huo kunaweza kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira usioweza kurekebishwa, na kufanya kesi hiyo kukosa maana iwapo walalamishi wataibuka washindi. Mary Muoki ana taarifa zaidi.