- 4,315 viewsDuration: 3:26Mamake mchanganuzi wa masuala ya usalama aliyetoweka Mwenda mbijiwe, aliangua kilio nje ya mahakama baada ya kesi ya kuwataka maafisa wa polisi kumwasilisha mwanawe akiwa hai au mfu kutupiliwa mbali. Mahakama Kuu imetupilia mbali kesi iliyowasilishwa na familia Mbijiwe ikisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa alitoweka akiwa mikononi mwa maafisa wa usalama. Jaji Martin Muya alisema ilikuwa jukumu la familia ya Mbijiwe kuthibitisha madai hayo na japo ilifanikiwa kuonyesha kuwa alikamatwa na polisi kabla ya kutoweka, haikuthibitisha kuwa aliendelea kusalia mikononi mwa polisi baadaye.