Skip to main content
Skip to main content

Maiti moja imepatikana baada ya jengo kuporomoka eneo la Oloolua, Kajiado

  • | Citizen TV
    387 views
    Duration: 1:34
    Maiti moja imepatikana kutoka kwenye jengo la ghorofa nane lililoporomoka katika eneo la Olenairi, Oloolua, Kajiado Kaskazini huku juhudi za kuwatafuta watu wengine watatu zikiingia siku ya tatu. Naibu Kamishna wa Kajiado Kaskazini Yusuf Mohammad amesema shughuli za uokoaji zimetatizwa baada ya sehemu nyingine ya jengo hilo kuonyesha dalili za kuporomoka, hali inayowaweka hatarini maafisa wa uokoaji. Amewarai familia zilizoathirika pamoja na wananchi kuwa na subira akisema maafisa kutoka idara mbalimbali wanaendelea na operesheni hiyo kwa tahadhari kubwa ili kuhakikisha usalama.