- 75,538 viewsDuration: 2:35Mamia ya Wakenya wameendelea kumiminika katika nyumba moja katika kijiji cha Emenwa, eneobunge la Bobasi, kaunti ya Kisii, kufuatia ripoti za madai ya kuonekana kwa kivuli cha Maria, mamake Yesu, kwenye boma hilo. Baadhi ya wakazi wanadai kuona picha hiyo ukutani, huku wengine waliofika wakisema hawakuona chochote. Polisi eneo hilo wamelazimika kudhibiti umati wa watu waliofika Emenwa, kama Chrispine Otieno anavyoarifu.